Babu Owino akosoa uongozi wa Oburu Oginga katika ODM

Babu Owino akosoa uongozi wa Oburu Oginga katika ODM

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amekosoa uongozi wa Kinara wa Chama cha ODM Dkt Oburu Oginga na kumtaka kuukabidhi uongozi wa Chama hicho kwake.

Owino amemtaka Oburu kuitisha mkutano wa kitaifa wa viongozi wote wa chama hicho ili kufanya uchaguzi wapya wa viongozi, akisema Chama cha ODM kinahitaji viongozi wenye malengo na wawajibikaji.

Akizungumza na Wanahabari jijini Nairobi, Owino alisema wakati umefika sasa wa Chama cha ODM kuongozwa na viongozi vijana ambao watahakikisha chama kinajenga msingi dhabiti mashinani na wala sio viongozi wazee.

Aidha alisisitiza kwamba siasa itaendelea jinsi zilivyo, huku akiweka wazi kwamba chama hicho kinahitaji viongozi vijana na wenye fikra pana.

“Wakati sasa wa chama cha ODM kuitisha mkutano wa kitaifa wa viongozi wote wa chama hicho ili kufanya uchaguzi wapya wa viongozi na kwamba Kiongozi wa chama anafaa kupewa babu Owino, alisema Owino.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi