Murkomen: Serikali imefikia asilimia 70 ya wanafunzi kujiunga na gredi ya 10

Murkomen: Serikali imefikia asilimia 70 ya wanafunzi kujiunga na gredi ya 10

Serikali kuu imesema imefikia asilimia 70 ya wanafunzi wanaojiunga na shule za gredi ya 10 kote nchini ili kuhakikisha hakuna wanafunzi anasilia nyumbani.

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen aliwataka maafisa tawala ikiwemo machifu na manaibu wao kuhakikisha wanafunzi waliomaliza gredi ya 9 wanajiunga na shule za sekondari ya juu ili kufanikisha malengo yao.

Waziri Murkomen alisema serikali iko tayari kutafuta ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kote nchini ili kuhakikisha agizo la rais la wanafunzi wote waliomaliza gredi ya 9 wanajiunga na shule za sekondari ya juu ama gredi ya 10 linatimizwa.

Aidha alidokeza kwamba Wizara ya elimu nchini iliongeza mda wa wanafunzi wanaojiunga na gredi ya 10 ili kupiga jeki sekta ya elimu na kuwawezesha wanafunzi wanatimiza ndoto yao masomoni.

“Wizara ya elimu iliongeza mda wa wanafunzi ambao hawakutayari kujiunga na gredi ya 10 wazazi wao wanakamilikisha huo mpango na watoto hao wanaingia shule ili kuhakikisha kunafikia ile asilimia 100 ya wanafunzi kujiunga na shule kote nchini”, alisema Waziri.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi