Maafisa wa usalama mjini Malindi kaunti ya Kilifi wamewakamata washukiwa 18 kwenye msako uliolenga magenge ya kihalifu yaliyokuwa yakiwahangaisha wakaazi wa eneo hilo.
Oparesheni hiyo ilifanyika eneo la Muyeye na Milano ambapo washukiwa hao walikamatwa wakiwa na simu za wizi, runinga na silaha zinazoaminika kutumika kutekelezea uhalifu.
Washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi wakitarajiwa kufikishwa mahakamani.
Idara ya usalama imetoa onyo kali kwa wakaazi ambao wanaendelea kuwaficha wahalifu ikizingatiwa kwamba wahalifu hao wanaishi miongoni mwao.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
