Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama barabarani, NTSA, imetoa tahadhari ya kiusalama ikiwataka madereva na watumiaji wengine wa barabara kuwa waangalifu kutokana na mvua kubwa na ukungu unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Katika taarifa yake iliyotolewa NTSA ilisema hali ya hewa inayoshuhudiwa kwa sasa imezidisha kwa kiwango kikubwa hatari katika barabara kuu nchini.
NTSA iliwashauri watumiaji wa barabara kupunguza mwendo, kudumisha umbali kati ya magari, kuepuka kupita magari mengine endapo kuna ukungu, pamoja na kuwa makini na maeneo yenye maji mengi hasa katika barabara za maeneo ya tambarare.
Onyo hilo linajiri kufuatia tahadhari ya idara ya hali ya hewa iliyoeleza kuwa maeneo kadhaa yanatarajiwa kupokea mvua ya wastani hadi ya zaidi ya milimita ishirini hadi thelathini.
Maeneo hayo ni pamoja na nyanda za chini za kusini mashariki, nyanda za juu za mashariki na magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Victoria pamoja na sehemu za Pwani
