News

Mwanamke Amefariki kwa Ajali ya Barabarani, Kwale

Published

on

Mwanamke mmoja amethibitishwa kufariki huku watu wengine sita wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Matairini kwenye barabara kuu ya Kwale – Kombani katika kaunti ya Kwale.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu hao walikuwa wameabiri matatu kuelekea mjini Kwale kabla ya matatu hiyo kugongana ana kwa ana na gari aina ya Landcruiser la maafisa wa idara ya upepelezi nchini DCI.

Wakaazi wa maeneo hayo, wamesema gari la maafisa wa DCI lilipoteza muelekeo na kusababisha ajali hiyo, wakiwalaumu madereva wa magari ya maafisa wa usalama kwa kuendesha magari hayo kwa mwendo wa kasi.

Akizungumzia ajali hiyo Afisa mkuu wa polisi eneo la Matuga Alex Chepsoi amesema tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini iwapo gari hilo la DCI lilikuwa linaendeshwa kwa kasi ili kumchukulia hatua za kisheria dereva husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version