News
Mung’aro: Hospitali ya Kilifi Inaidai SHA Shilingi Milioni 130
Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro amebainisha kwamba hospitali kuu ya rufaa ya Kilifi inaidai bima ya afya ya jamii nchini SHA jumla ya shilingi milioni 310.
Gavana Mung’aro ameyasema hayo mbele ya kamati ya uwekezaji katika bunge la Seneti ambapo amesema deni hilo limetatiza utoaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo japo serikali yake imekuwa ikiendeleza juhudi za kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu yanayostahili.
Gavana Mung’aro amefichua kwamba serikali ya kitaifa imekuwa ikikosa kulipa fedha hizo kwa muda mrefu na kulitaka bunge la Seneti kuliangazia suala hilo ili malipo ya deni hilo la SHA yaweze kufanyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Seneti Godfrey Osotsi amekiri kupokea lalama hizo na kuahidi kwamba suala hilo litashughulikia kikamilifu na bunge la Seneti ili kufanikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.