News
Mudavadi: Uhusiano wa Kenya na Marekani uko imara
Waziri wa Masuala ya kigeni Musalia Mudavadi amepuuzilia mbali madai kuwa uhusiano kati ya Kenya na Marekani unayumba.
Hii ni kufuatia mswada uliowasilishwa katika bunge la Congress na seneta James Risch wa Marekani.
Risch alipendekeza Kenya ipokonywe hadhi yake ya mshirika asiye mwanachama wa NATO akitaja hatua ya Kenya kujihusisha zaidi na Uchina.
Pendekezo lengine ni pamoja na tuhuma za Kenya kushirikiana na kundi la waasi wa RSF nchini Sudan.
Mudavadi alisisitiza mswada huo sio msimamo wa serikali ya Marekani, akishikilia kuwa uhusiano wa Nairobi na Washington unasalia imara.
Taarifa ya Joseph Jira.