Sports
Mshambulizi Wa Nigeria Victor Osimhen Asajiliwa Na Galatasaray
Mabingwa wa Ligi Kuu Uturuki, Galatasaray wamekamilisha usajili wa mshambuliaji, Victor Osimhen, 26, raia wa Nigeria kwa ada ya uhamisho ya jumla ya Euro milioni 75 zitakazolipwa kwa awamu akitokea Napoli Napoli.
Osimhen ambaye msimu uliopita alikuwa Galatasaray kwa mkopo akitokea Napoli sasa anarejea jumla klabuni kwa mkataba wa miaka mitatu utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2028.
Kwenye mkataba huo Napoli imeiwekea Galatasaray sharti la kutomuuza nyota huyo kwenda klabu yoyote ya Serie A kwa kipindi cha miaka miwili vinginevyo itakumbaka adhabu ya malipo ya ziada.
#Kpenga