News

Msaidizi wa mbunge wa Kilifi Kusini afikishwa Mahakamani.

Published

on

Mahakama ya Shanzu, Kaunti ya Mombasa, imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili au pesa taslimu ya shilingi laki moja msaidizi wa kibinafsi wa Mbunge wa Kilifi Kusini.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyowasilishwa mahakamani, mnamo Juni 3, mwaka 2024, katika eneo la Half London, Majengo, Kanamai, Kaunti ya Kilifi, Victor Katana Mganga pamoja na wenzake ambao hawakufika mahakamani, walidaiwa kushirikiana kubomoa ukuta kinyume cha sheria, mali ya Duncan Mkala Kumbe.

Aidha, Katana anakabiliwa na shtaka la pili ambapo inadaiwa kuwa mnamo Juni 21, mwaka 2024, katika eneo hilo hilo la Half London, Majengo, Kilifi Kusini, pamoja na washukiwa wengine ambao pia hawakuwa mahakamani, walishirikiana kubomoa ukuta mwingine wenye thamani ya shilingi milioni sita, mali ya Kassim Abdalla Mohammed.

Hata hivyo, Katana amekana mashtaka yote mawili dhidi yake.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version