News

Mpango wa Skills Mtaani kufaidi vijana 600 Malindi.

Published

on

Jumla ya vijana 600 kutoka eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi watanufaika na mpango wa mafunzo ya taaluma za ujuzi, maarufu SKILLS MTAANI unaofadhiliwa na mbunge wa Malindi Amina Mnyazi.

Akizungumza na wanahabari mjini humo, Mnyazi alidokeza kuwa mpango huo utakaotekelezwa kupitia vyuo vya kiufundi vilivyo katika eneo hilo unalenga vijana walio mitaani ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kujistawisha.

Mnyazi alikariri kuwa mpango huo pia utasaidia kupunguza visa vya utovu wa usalama vinavyoshuhudiwa mjini humo kwa kuwapa vijana ujuzi wa kujishughulisha katika jamii.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi kutoka eneo la Kijiwetanga wakiongozwa na Esther Mathias na Katao Nzai Joseph waliupongeza mpango huo wakisema utasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na kupunguza uhalifu katika jamii.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version