Sports

Morocco Kukosa Nyota Wanne Kombe La CHAN

Published

on

12 DAYS TO GO CHAN-Siku 12 zikiwa zimesalia kungoa nanga taji la CHAN Tumulike Mabingwa mara 2 wa kombe hilo Morocco.

Morocco-Wanajiita The Atlas Lions kwa jina la Utani
Wameshiriki kombe la CHAN mara 4 (2014, 2016, 2018, 2020)
Kocha mkuu ni :Tarik Sektioui ambaye amewahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa hilo na kwa sasa ananoa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23.

Taifa hilo pamoja na DR.Congo watakua wanalenga kuingia kwenye daftari za Kumbukumbu kwa kuwa taifa la kwanza kushinda taji hilo mara tatu,Morocco wakiwa wameshinda mara 2 mwaka 2018 na 2020.

Baadhi ya wachezaji wakuangaziwa kwenye kikosi cha timu hiyo ni pamoja na nyota Bouchaïb Arrasi wa kilabu ya Raja Casablanca pamoja na Younes El Kaabi wa Racing Casablanca.

Mwalimu huyo hata hivyo atakosa wachezaji wanne ambao wote wamepata vilabu vya nje,wachezaji hao ni pamoja na;Amin Zahzouh, Akram Al-Naqqash, Hatem Al-Sawabi, and Adel Tahaif.
The Atlas Lions wako Kundi A pamoja na Kenya,Angola,Zambia na DR.Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version