Business
Mombasa Yapoteza Watalii kwa Zanzibar, Waziri Ataka Mageuzi
Waziri wa Utalii, Utamaduni na Biashara katika Kaunti ya Mombasa, Mohammad Osman, amesema sekta ya utalii imekuwa ikidorora katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo huenda ikaathiri uchumi wa kaunti hiyo.
Akizungumza na wanahabari, jijini Mombasa waziri Osman ameitaka serikali kufungua anga za Kenya kuwa huru kwa mashirika ya ndege ya kimataifa, ili kuongeza idadi ya watalii wanaowasili humu nchini .
Kwa mujibu wa waziri huyo, kwa muda mrefu Mombasa imekuwa ikishindana na Zanzibar kama kivutio kikuu cha watalii Afrika Mashariki, ila mwaka jana Zanzibar ilipokea zaidi ya watalii 800,000 huku Mombasa ikipokea takribani 200,000 pekee.