Sports

Mo Salah Aibuka Mchezaji Bora wa PFA kwa Mara ya Tatu, Baada Ya Kuiongoza Liverpool Kutwaa Taji

Published

on

Mahambulizi wa Liverpool Mohamed Salah ametangazwa Mchezaji Bora wa Wachezaji wa PFA (PFA Players’ Player of the Year) baada ya msimu wa kihistoria wa 2024-25 ambapo alishinda taji la ligi na Liverpool, akifunga mabao 29 na kushinda kiatu cha dhahabu (Golden Boot) kwa mara ya nne.

Idadi yake ya juu zaidi ya pasi za mabao msimu uliopita, 18, ni rekodi bora zaidi katika historia ya Premier League ikizidiwa tu na Kevin de Bruyne na Thierry Henry.

Mwanasoka huyo kutoka Misri pia amekuwa mchezaji wa kwanza kabisa kushinda tuzo hiyo mara tatu, na vilevile ameorodheshwa kwenye Kikosi cha Mwaka cha Premier League akiwa na wachezaji wenzake watatu – Virgil van Dijk, Ryan Gravenberch na Alexis Mac Allister.

Salah alipokea tuzo hiyo mikononi mwa Ian Rush, mfungaji bora wa muda wote wa Liverpool. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alishinda kura mbele ya Mac Allister, Bruno Fernandes, Alexander Isak, Cole Palmer na Declan Rice.

Katika kikosi bora cha msimu wa mwaka msimu jana;

Matz Sels (Nottingham Forest)

William Saliba (Arsenal)

Gabriel (Arsenal)

Virgil van Dijk (Liverpool)

Milos Kerkez (Bournemouth, now Liverpool)

Declan Rice (Arsenal)

Alexis Mac Allister (Liverpool)

Ryan Gravenberch (Liverpool)

Mohamed Salah (Liverpool)

Chris Wood (Nottingham Forest)

Alexander Isak (Newcastle)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version