News

Misitu ya Kaya Hatarini

Published

on

Mwenyekiti wa Shirika la Malindi District Cultural Association, MADCA Stanley Kahindi Kiraga amesema misitu ya Kaya iko katika hatari ya kuangamizwa licha ya kuwa misitu hiyo ni muhimu kwa jamii.

Kiraga alisema misitu hiyo ni mojawapo ya vyombo vinavyotumika kuhifadhi turathi na mila za jamii ya Mijikenda kwenye kaunti za Kilifi na Kwale.

Akizungumzia mpango wa kutumika kwa takriban ekari tatu katika kufanikisha mradi wa maendeleo kwenye msitu wa Kaya fungo katika kaunti ya Kilifi, Kiraga alipinga vikali mpango huo.

Kwa upande wake Afisa wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Tema Digital Research Trust, Eric Mgoja alikashifu kuingiliwa kwa misitu ya Kaya akisema ni ukiukaji mkubwa wa mila na desturi za kijamii ikizingatiwa kwamba misitu hiyo ni ya kiasili.

“Ni wakati sasa wa wazee wa kaya na wanajamii wa Mijikenda kushirikiana ili kuhakikisha kuwa ardhi za misitu ya kaya zinasajiliwa kisheria”, alisema Mgoja.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Shirika la utetezi wa haki za ardhi nchini Kenya Land Alliance, Faith Alubbe alisema suala hilo litasaidia katika kulinda na kuhifadhi misitu ya Kaya dhidi ya wanyakuzi.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version