News
Miili mingine 4 yapatikana kwa Binzaro- Shakahola
Mili mingine minne imepatikana ikiwa imeoza kiasi cha kutotambulika katika msitu wa Shakahola karibu na kijiji cha Binzaro eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Mili hiyo ilipatikama na wenyeji waliokuwa wakiendelea na shughuli zao katika msitu huo ambao umegonga vichwa vya habari tangu sakata ya Mhubiri tata Paul Mackenzie.
Kupatikana kwa miili hiyo ilisababisha idadi ya maiti zilizopatikana katika kisha cha hivi punde kabisa cha mauaji kwenye kijiji cha Binzaro kufikia Miili minane.
Maafisa wa usalama wanatarajiwa kukusanya mabaki ya hayo ili kuyapeleka katika makafani ya hospitali ya Malindi ambako
miili mingine iliyopatiakana katika kisa cha kwanza cha mauaji ya Shakahola ‘One’ inahifadhiwa.
Majuma mawili yaliyopita, Maafisa wa Polisi walivamia msitu huo na kupata maiti nne na makaburi sita ambayo sasa yanasubiri kufukuliwa.
Wahusika waliokuwa wakiendesha mafunzo ya itikadi kali katika eneo hilo lenye vijumba vitamo, waliwahi kutoroka wakiacha maiti moja ambayo ilikuwa haijazikwa.
Shughuli za kufukua makaburi hayo bado haijafanyika huku eneo hilo la msitu wa Kwa Binzaro likiwekwa chini ya ulinzi wa maafisa wa usalama.
Msako dhidi ya maafisa hao bado unaendelea katika msitu huo wa Shakahola.
Mackenzie na wenzake 30 walikamatwa na sasa wanasubiri kukamilika kwa kesi yake inayoendeshwa katika Mahakama za mjini Mombasa.
Taarifa ya Eric Ponda