Sports

Mbeumo Akabidhiwa Jezi Namba 19 United, Baada Ya Kuzinduliwa Rasmi

Published

on

Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji, Bryan Mbeumo kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 71 pamoja na nyongeza akitokea Brentford na atavaa jezi namba 19 klabuni hapo.
Mbeumo (25) raia wa Cameroon amemwaga wino kwa mkataba wa miaka mitano utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2030 na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi.
Msimu uliopita nyota huyo alikuwa mfungaji bora namba nne kwenye Ligi Kuu England nyuma ya Salah (29), Isak (23) na Haaland (22) akipachika jumla ya magoli 20 na kusaidia ‘assists’ mengine 8.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha Ruben Amorim baada ya usajili wa mshambulizi Matheus Cunha kutoka kilabu ya Wolves.
#Kipenga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version