News
Mahakama Yaagiza Washukiwa wa Ubakaji Kuzuiliwa Rumande
Mahakama ya Kilifi imeagiza kuzuiliwa rumande washukiwa wawili wa kesi ya ubakaji wa msichana wa umri wa miaka 16, kaunti ya Kilifi.
Hakimu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa ameagiza washukiwa wa kesi hiyo akiwemo Gift Kalu na Emmanuel Mganga kuendelea kuzuiliwa rumande hadi tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
Awali kabla ya agizo hilo, Mahakama ameelezwa kwamba washukiwa hao walitekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 9 mwezi Aprili mwaka huu katika kijiji cha Mwembetsungu katika kaunti ya Kilifi.
Mahakama pia imeelezwa kwamba wawili hao walitekeleza unyama huo baada ya kumshika shingo na mdomo msichana huyo na kisha kumsukuma kichakani alipokuwa ametoka kuanua viatu nje ya nyumba.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu.