Connect with us

Sports

Mabondia Kutoka Vilabu Mbalimbali Nchini, Kuzindua Uhasama Mjini Mombasa

Published

on

Zaidi ya mabondia 180 wa kiwango cha juu kutoka vilabu 26 kote nchini wanatarajiwa kushiriki mashindano ya ndondi ya mzunguko wa pili Kenya yanayotarajiwa kuanza hii leo hadi 19 mwaka huu yatakayoandaliwa katika taasisi ya Alliance Francaise jijini Mombasa.

Miongoni mwa mabondia watakaoshiri mashindano hayo ni Bonface Mogunde wa huduma ya polisi nchini ambaye hajapoteza pambano katika uzani wake, mshindi wa dhahabu kwenye Michezo ya Afrika Edwin Okongo wa KDF mabondia wa Mombasa, Kombo Mwinyifaki na Shaffi Bakari, pia watapanda ulingoni.

Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha Ndondi cha Kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na taasisi ya Alliance Française kama sehemu ya mradi wa ushirikiano wa michezo kati ya Kenya na Ufaransa uitwao Ndondi Mashinani, kwa usaidizi wa Ubalozi wa Ufaransa.

Michuano hiyo inalenga kukuza vipaji, hasa kwa wanawake na vijana, pamoja na kuandaa wawakilishi wa Mombasa kwa mashindano ya Olimpiki yajayo.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.   

Published

on

By

Huku zikiwa zimesalia siku 15 pekee kung’oa nanga kwa kipute cha CHAN mwezi ujao,
Kenya imeratibiwa kupambana na DRC, Morocco, na Angola katika Kundi A linalotajwa kuwa ndio kundi gumu zaidi yaani Kundi la Kifo.
KUNDI B
Ni Taifa jirani la Tanzania, Burkina Faso, Madagascar na Jamhuri ya Africa ya Kati.
KUNDI C
Uganda itachuana na Algeria,Africa Kusini,Guinea na Nigeria.
KUNDI D:
Congo itakabana koo na Nigeria,Senegal na Sudan Kusini.
 Mechi hizi zitasakatwa katika nyuga za katika Kenya, Uganda na Tanzania,
Continue Reading

Sports

Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Published

on

By

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.

Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.

Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.

Continue Reading

Trending