Business
Maandalizi ya maonyesho ya Kilimo Mombasa yaanza.
Wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi wamehimizwa kushiriki kikamilifu kwenye maonyesho ya kilimo yatakayofanyika mwezi wa september mwaka 2025 katika uwanja wa maonyesho ya kilimo jijini Mombasa.
Mwenyekiti wa maandalizi ya maonyesho hayo eneo la pwani Henry Nyaga alisema hatua hiyo itawasalidia wakulima na wafanyabiashara kubadilishana maarifa na uzoefu katika nyanja ya kilimo-biashara.
Nyaga aidha alieleza kuwa mwaka huu 2025 kutakuwa na ushirika wa wadau wapya kutoka ndani na nje ya nchi.
Alidokeza kuwa masuala ya uchumi wa raslimali za bahari na maziwa yatapewa kipaumbele katika maonyesho hayo.
Taarifa ya Pauline Mwango