News
K’opolo: Wanasiasa Wasiingilie Masuala ya Elimu
Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET kimekosoa wanasiasa kwa kuingilia masuala ya walimu nchini hasa kupandishwa vyeo kwa walimu.
Naibu Katibu wa KUPPET tawi la kaunti ya Kilifi Opolo K’opolo amesema walimu wanapitia changamoto nyingi na suala hilo halifai kuingiziwa siasa.
Akizungumza na Coco Fm K’opolo amesema wabunge wana jukumu la kushinikiza mgao bora wa fedha kwa Tume ya kuajiri walimu nchini TSC ili maslahi ya walimu yaboreshwe pamoja na kuboresha viwango vya elimu nchini.
Wakati huo huo amekana madai ya kuwakandamiza walimu walio chini ya Chama hicho kupitia makato ya kila mara, akidai kwamba wanawahudumia vyema walimu.