News
Kijana wa Umri wa Miaka 15 Amejitoa Uhai Katika Kituo cha Polisi cha Bamba
Kijana wa umri wa miaka 15 ameripotiwa kujitoa uhai katika kituo cha polisi cha Bamba eneo bunge Ganze kaunti ya Kilifi, alipokuwa akizuiliwa.
Kulingana na taarifa ya maafisa wa polisi, kijana huyo alikuwa amezuiliwa tangu siku ya Ijumaa tarehe 18 mwezi huu kufuatia mzozo wa kimapenzi, hali ambayo ilisababisha wazazi wa msichana kuwasilisha ripoti kwa polisi.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba maafisa wa polisi walikuwa bado wanaendelea na uchunguzi wao kufuatia madai hayo na kushangazwa na hatua iliyochukuliwa na kijana huyo ya kujitoa uhai kwa kutumia shati lake ndani ya kituo hicho cha polisi.
Maafisa wa polisi wamesema wamebaini mauti hiyo wakati polisi walipokuwa wakiendelea na doria katika kituo hicho cha polisi, japo wamesema wameanzisha uchunguzi zaidi kubaini kilichosababisha kijana huyo kujitoa uhai.
Hata hivyo mwili wa kijana huyo umpelekwa katika hifadhi ya maiti huku wananchi wakikosoa jinsi maafisa wa usalama wanavyoshuhulikia kesi za mizozo ya kimapenzi, matatizo ya afya ya akili na uhalifu.