Sports

KCB Watawala Christie Sevens kwa Ushindi wa Taji Kuu

Published

on

Kilabu ya wanabenki KCB cha raga walitwaa ubingwa wa toleo la 59 la Christie Sevens baada ya kuwazidi nguvu Menengai Oilers kwa alama 26–7 katika fainali ya Main Cup iliyopigwa Jumapili kwenye uwanja wa RFUEA Grounds jijini Nairobi.

Wanabenki, hao ambao wamekuwa kwenye viwango vya juu msimu huu, walipiga hatua ya kwanza kupitia Floyd Wabwire aliyepenya ngome ya Oilers na kugusa chini katikati ya nguzo, kisha Brian Wahinya akakamilisha kwa mikwaju na kuwapa uongozi wa 7–0.

Festus Shiasi aliongeza try ya pili na kupanua uongozi wa KCB, ingawa mkwaju wa Wahinya haukuingia, na kupelekea timu kuingia mapumziko wakiwa mbele kwa alama 12–0. Baada ya kipindi cha pili kuanza, Wabwire alionesha kasi yake tena kupitia mbinu ya kick-and-chase na kufunga try jingine, ambalo Wahinya alilibadilisha na kuongeza alama, na kufanya uongozi kuwa 19–0.

Oilers, waliokuwa wameindoa Strathmore Leos katika nusu fainali ya kusisimua, walijibu kupitia Samuel Mwaura, ingawa mkwaju wake haukuingia.

Hata hivyo, KCB hawakusita, Waliendeleza mashambulizi na kufunga try lingine la mwisho, ambapo Wahinya aliongeza mkwaju kwa ustadi na kukamilisha ushindi wa 26–7, na hivyo kuipatia KCB taji la heshima la Christie Sevens.

Mapema, Strathmore Leos walishika nafasi ya tatu baada ya kuilaza Kenya Harlequins 24–19 kupitia muda wa sudden-death, Gabriel Ayimba akihitimisha mchezo huo kwa try la ushindi.

Kabras Sugar walinyakua nafasi ya tisa baada ya kuibwaga Mwamba 12–7, huku Nondescripts wakifunga nafasi ya tano kwa kuichapa Impala RFC 28–17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version