Business
KAHC: Kenya Yaweza Kukosa Watalii Milioni 5 Kufikia 2027
Muungano wa wahudumu wa hoteli na wapishi nchini (KAHC) umesema huenda Kenya ikakosa kufikia lengo la watalii millioni 5 ifikapo mwaka 2027 iwapo maandamano yanayoshughudiwa mara kwa mara humu nchini hayatasitishwa.
Kwa mujibu wa viongozi wa muungano huo, maandamano hayo yamewafanya wageni wengi kutoka mataifa ya kigeni kusitisha safari zao za kuzuru Kenya, hali inayoathiri sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki wa Hoteli na Mikahawa nchini (KAHC) Chris Musau, anasema kuwa taswira ya nchi kimataifa imeathirika, na hali hiyo inaweza kupunguza mapato ya sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya fedha za kigeni kwa taifa.
Musau aidha anaitaka serikali kuanzisha mazungumzo na vijana wa kizazi cha Gen Z kutafuta suluhu ya migogoro iliyopo ili kurejesha hali ya utulivu nchini.