Sports

Junior Strikers Mchezo Wa Voliboli Warejea Nchini na Kombe la Afrika

Published

on

Kikosi cha voliboli kwa chipukizi Junior Strikers kimerejea nchini asubuhi ya leo kutoka Yaoundé, Cameroon, baada ya kutwaa kombe la Ubingwa wa Afrika kwa chipukizi kwa kuwalaza wenyeji Cameroon seti 3–1 kwenye fainali iliyochezwa jana.

Kikosi hicho, kinachoongozwa na kocha Jacklyne Juma, kiliwasili alfajiri na kulakiwa na Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Voliboli Kenya (KVF), Paul Bitok, ambaye aliwapongeza wachezaji hao kwa kupeperusha kwa heshima bendera ya taifa la Kenya.

Junior Strikers walitinga fainali baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3–0 (25–19, 25–19, 25–23) dhidi ya Misri katika nusu fainali, huku Cameroon wakiwatoa Senegal seti 3–0 kwenye nusu fainali nyingine.

Kenya ilipoteza mechi moja pekee katika mashindano hayo — dhidi ya wenyeji Cameroon kwa seti 3–1 — kabla ya kushinda mechi zingine nne. Mashindano hayo yalihusisha jumla ya mataifa sita: Cameroon, Senegal, Misri, Burundi, Uganda na Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version