Sports

Junior Strikers Mabingwa Wa Afrika Mchezo wa Voliboli

Published

on

Kikosi cha voliboli cha wanawake chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, maarufu kama Junior Strikers, kimetwaa ubingwa wa Mashindano ya Afrika kwa Chipukizi yaliyokamilika jana mjini Yaoundé, Cameroon.

Hii ni baada ya warembo hao kuwalaza wenyeji Cameroon kwa seti 3–1 katika fainali kali iliyopigwa jana mjini humo.

Junior Strikers walishinda kwa seti za 26–24, 19–25, 28–26 na 25–16, na hivyo kulipiza kisasi baada ya kupoteza mechi moja pekee dhidi ya wenyeji hao katika hatua ya mzunguko.

Mchezaji nyota Terry Tata Mallin alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano, huku akishinda pia tuzo ya mchezaji bora wa mchezo dhidi ya timu za Misri, Senegal, Burundi na Uganda.

Mchezaji wa nafasi ya nje Milka Akinyi naye alituzwa kama mchezaji bora wa kuzuia mashambulizi ya wapinzani.

Mashindano hayo, yaliyodumu kwa wiki moja, yalihusisha mataifa ya Cameroon, Kenya, Uganda, Burundi, Misri na Senegal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version