News
Juhudi za kuokoa Ndovu waliokwama matopeni zaendelea Jaribuni
Maafisa wa huduma kwa wanyamapori nchini KWS wanaendelea na juhudi za kuwaokoa Ndovu wawili waliokwamwa kwenye Matope katika eneo la mkono wa bahari kwenye eneo la Kauma-Jaribuni kaunti ya Kilifi.
Ndovu hao wanasemekana kutoka mbuga ya wanyama ya Tsavo na wamekuwa wakihangaisha wakaazi eneo hilo na kuharibu mimea ya wakulima.
Kulingana na wakaazi hao, Ndovu wengine watatu walikuwa wakizurura katika vijijini vya eneo hilo na kuendelea kuharibu mimea yao mashambani.
Kufikia jana jioni maafisa wa KWS walifika eneo hilo wakiwa na ndege aina ya Helkopta wakitafuta mbinu za kuwaokoa wanyama hao waliokuwa wanaendelea kudidimia kwenye matope.
Wakaazi wao wanashinikiza KWS kudhibiti wanyama hao ili kuepuka mimea zaidi kuharibiwa zaidi.
Taarifa ya Mwanahabari wetu