News
Jaji mkuu mstaafu Maraga akosoa serikali ya Rais Ruto.
Jaji Mkuu mstaafu David Maraga ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa utawala wa rais William Ruto kufuatia kifo cha mwanablogu Albert Omondi Ojwang anayedaiwa kufariki akiwa mikononi mwa maafisa wa polisi.
Katika taarifa yenye maneno makali iliyotolewa Maraga, alinukuu ripoti ya upasuaji wa maiti ya mwanapatholojia wa serikali, ambayo anasema inathibitisha kuwa Ojwang alitendewa ukatili, kunyongwa, kuteswa na kuuawa na maafisa wa polisi.
Maraga ambaye anawania wadhfa wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2027, alikumbusha maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z, ambapo zaidi ya vijana 100 walipoteza maisha kutokana na ukatili wa maafisa wa polisi.
Vile vile alilaani utawala wa rais Ruto kwa kuunga mkono mauaji ya kiholela, akitaja kifo cha Ojwang’ kama tukio la mwisho.
Maragapia alishtumu serikali kwa kufumbia macho madai ya ugaidi unaofadhiliwa na serikali.
Wakati huo huo Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga aliagiza hatua za haraka kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa polisi waliohusika na mauaji ya kijana huyo huku akisistiza uwajibikaji.
Taarifa ya Joseph Jira