Sports

Hakuna Vilabu Vya Kenya,Vilabu 100 Bora Barani Afrika Orodha Ya CAF

Published

on

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya vilabu bora Afrika kwa viwango vya CAF ambapo Klabu ya Simba Sc ya Tanzania imeendelea kusalia kwenye 10 bora (Top ten) ikishikilia nafasi ya tano nyuma ya vinara Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance Tunis na RS Berkane.

Orodha hiyo imetoka kuelekea droo ya hatua ya michuano ya CAFCL na CAFCC itakayofanyika Agosti 9, 2025 ambapo Tanzania imeingiza timu tatu kwenye orodha ya vilabu 100 bora barani humo ikiwemo Simba Sc (pointi 48) iliyopo nafasi ya 5, Yanga Sc (pointi 34) iliyopo nafasi ya 12 na Namungo Fc (pointi 0.5) iliyopo nafasi ya 75 ikifungana kwa pointi na vilabu vingine 5.
Hakuna timu yoyote kutoka Kenya iliyoingia kwenye vilabu 100 bora barani Afrika huku Simba Sc ikishikilia usukani kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, Yanga Sc nafasi ya pili, Vipers ya Uganda nafasi ya tatu na Namungo Fc nafasi ya nne na ndio vilabu vinne pekee vilivyopo kwenye top 100 ya CAF kutoka CECAFA.
VILABU 10 BORA AFRIKA:
1.  Al Ahly (pointi 78)
2.  Sundowns (62)
3.  Esperance (57)
4.  Berkane (52)
5.  Simba Sc (48)
6.  Pyramids (47)
7.  Zamalek (42)
8.  Wydad AC (39)
9.  USM Alger (37)
10.  CR Belouizdad (36)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version