News
Gachagua, Asema maisha yake yako hatarini
Aliyekuwa Naibu rais Rigathi Gachagua amesema maisha yake yako hatarini kutokana na msimamo wake wa kisiasa nchini.
Katika barau aliyomuandikia Inspekta jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja na Rais William Ruto pamoja na vitengo vingine vya usalama nchini, Gachagua ameorodhesha baadhi ya matukio aliyonusurika kuuwawa.
Kiongozi huyo amevitaka vitengo husika vya usalama kuchunguza matokeo hayo na kuwatia nguvuni wahusika sawa na kupewa ulinzi wa hali ya juu.
Kauli sawa na hiyo imetolewa na Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natambeya ambaye amesema maisha yake yako hatari kwani amepata habari kuhusu kuwepo kwa njama dhidi yake kufuatia ukosoaji wake kwa serikali.