News

DCI, Wanachunguza Kifo Tatanishi cha Afisa wa Polisi

Published

on

Maafisa wa Idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI wanachunguza kisa kimoja ambapo afisa wa polisi katika kitengo cha msafara wa rais ameanguka na kufariki alipokuwa akiabiri gari eneo la Karen jijini Nairobi.

Kulingana na taarifa kutoka kwa maafisa wa DCI, Daniel Kipruto Kangogo ameaga dunia wakati alipokuwa akijaribu kupanda gari katika harakati za kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba afisa huyo amepelekwa katika hospitali ya Karen ambapo maafisa wa afya wamethibitisha kifo chake alipowasilishwa katika taasisi hiyo.

Kangogo alikuwa na maafisa wenzake wakati wa tukio hilo na chanzo cha kifo chake hakijabainishwa.

Mwili wake unahiofadhiwa katika makafani ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version