Business

Biashara ya Vinyago Yadorora Malindi Kufuatia Upungufu wa Watalii

Published

on

Wadau wa sekta ya utalii wanaojihusisha na uuzaji vinyago mjini Malindi kaunti ya Kilifi wanalalamikia kusambaratika kwa biashara zao kufuatia idadi ndogo ya watalii wanaozuru eneo hilo kwa sasa.

Wakiongozwa na Mwendwa Ndunda wadau hao wanasema kuwa idadi ya watalii hususan kutoka mataifa ya kigeni ni ya chini mno ikilinganishwa na hapo awali hali inayoathiri shughuli zao.

Ndunda aidha ameeleza matumaini ya kuimarika tena kwa sekta hiyo hivi karibuni wakati ambapo watalii wataanza kuzuru eneo hilo kwa wingi.

Ndunda amefichua kuwa awali kituo chao cha kibiashara kilikuwa kikipokea takriban watalii 400 kwa siku tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version