Sports
Bailey Ajiunga Rasmi na As Roma ya Italia Akitoka Aston Villa
Mshambulizi wa Aston villa Leon Bailey amekamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Villa Park kwenda klabu ya Roma ya Italia.
Winga huyo wa Jamaica amejiunga na kikosi hicho cha Italia kwa msimu wa 2025-26, huku mkataba huo ukiwa na kipengele cha kununua.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Villa mwaka 2021 akitokea klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa dau la pauni milioni 25 na kufunga jumla ya magoli 22 katika mechi 144.
Bailey alifunga magoli 14 msimu wa 2023-24 katika mashindano yote, kiwango bora zaidi katika taaluma yake, lakini msimu uliopita alifunga mara mbili pekee katika michezo 38.
Alisaini mkataba mpya na Villa mnamo Februari 2024 ambao unatarajiwa kumweka klabuni hadi mwaka 2027.