National News

Asero: Unyanyapaa Dhidi ya Wagonjwa TB na HIV Ukomeshwe

Published

on

Wanaharakati wa maswala ya kiafya nchini wamehimiza umuhimu wa kuanzishwa kwa sera ambazo zitasaidia wagonjwa wa kifua kikuu yaani TB na virusi vya Ukimwi nchini ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Wakiongozwa na Eric Okioma kutoka Shirika la KELIN, Wanaharakati hao wamesema kuna haja ya serikali kuhakikisha inapotoa fedha kwa hazina ya bima ya Afya ya Taifa Care chini ya Mamlaka ya afya ya jamii SHA inazingatia pia watu wanaougua maradhi ya TB.

Wakizungumza na Wanahabari jijini Nairobi, Wanaharakati hao wameelezea wasiwasi wao kuhusu changamoto zinazowakumba wagonjwa hao, wakisema kuna haja ya sera muhimu kuanzishwa ili kuwasaidia wagonjwa wa TB na Ukimwi nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la kimataifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya HIV Patricia Asero ameshinikiza kukomeshwa kwa unyanyapaa dhidi ya wagonjwa TB na HIV ikiwemo maeneo ya shule na kazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version