News
Alube: Asilimia kubwa ya wakaazi wa Tanariver hawana ufahamu wa ardhi
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Kenya Land Alliance, Faith Alubbe amesisitiza haja ya serikali za kaunti na ile ya kitaifa kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi mashinani kuhusu haki za umiliki wa ardhi.
Alubbe aliema hatua hiyo itajenga jamii yenye ufahamu kuhusiana na masuala ya ardhi lakini pia itachangia kukabiliana na mizozo ya ardhi.
Akiongea mjini Hola, mkurugenzi huyo alikiri kuwa ufahamu wa wananchi kuhusu haki za ardhi katika kaunti ya Tanariver bado upo chini.
Alubbe alitoa wito kwa serikali zote kushirikisha jamii katika maswala yanayofungamanana ardhi.
Kwa upande wake mshirikishi wa Kenya land Alliance, kaunti ya Tanariver, Said Ilu aliitaka serikali kuhakikisha jamii za eneo hilo zinasajili ardhi zao hasa zile za kijamii.
Taarifa ya Hamis Kombe