Sports
Crystal Palace Mabingwa Ngao La Jamii
Kilabu ya Crystal Palace ndio mabingwa wa taji la Ngao ya Jamii marufu kama FA Cup Community Shield mechi iliopigwa hapo jana ugani Wembley.
Haya yanajiri baada ya The Eagles kushinda magoli 3-2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya magoli 2-2 muda wa kawaida.
The Reds walichukua uongozi kupitia kwa mshambulizi Hugo Ekitite dakika ya 4 kabila ya Palace kusawazisha kupitia kwa mshambulizi Jean Phillipe Mateta dakika ya 17 ,Hata hivyo kilabu hiyo ilichukua tena uongozi kupitia kwa beki Jeremie Frimpong dakika ya 21.
Goli la Ismael Sarr dakika ya 77 ilihakikisha mechi hiyo inamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.
Liverpool ikipoteza penalti zake kupitia Mohammed Salah,Alexis Mc Alister,na Harvey Elliot.
Crystal walijipatia magoli yake kupitia wachezaji kwa Jean Phillipe Mateta,Ismael Sarr na Justin Devenny
The Reds wanafungua ligi kuu Uingereza Ijumaa dhidi ya Afc Bournemouth.