Sports

Winga Wa Manchester United Garnacho Ataka Chelsea Pekee

Published

on

Klabu ya Chelsea imeafikia makubaliano ya maslahi binafsi ya kumsajili winga Alejandro Garnacho kutoka Manchester United huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 akitamani kujiunga na Mabingwa hao wa Dunia.

Chelsea imefungua mazungumzo na Manchester United juu ya kumsajili winga huyo ingawa kuna utofauti wa thamani kati ya timu hizo huku Mashetani Wekundu wakitaka kiasi kisichopungua pauni milioni 50 kumwachia nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid.

Garnacho 21, raia wa Argentina alionesha dhamira ya kujiunga na Chelsea tangu Julai huku akizikataa timu kutoka Italia na Ujerumani sambamba na kupiga chini ofa nono kutoka Saudi Arabia.
Tineja huyo amecheza mechi 144 akiwa na kilabu ya Manchester United huku akifanikiwa kufunga magoli 26 katika kipindi hicho ugani Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version