Business

Wafanyabiashara wa Matunda Malindi Walalamikia Kudorora kwa Biashara Kutokana na Ukosefu wa Soko

Published

on

Wafanyabiashara wa kuuza matunda karibu na soko la Kwa Jiwa mjini Malindi, Kaunti ya Kilifi, wanalalamikia kushuka kwa biashara yao kutokana na uhaba wa wateja katika eneo hilo.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Mshauri Mkuu wa chama cha Matunda Sales Group, Nathaniel Menza Chengo, amesema kuwa matunda yao yanaendelea kuharibika kila siku kwa kukosa wanunuzi, hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa biashara zao.

“Kwa sasa matunda ni mengi lakini hakuna soko. Tunapata hasara kubwa kwa sababu matunda yanaharibika kabla hatujayauza,” amesema Chengo.

Chengo ameitaka serikali ya kitaifa pamoja na serikali ya Kaunti ya Kilifi kuchukua hatua za haraka kwa kujenga kiwanda cha kusindika matunda ili kuwawezesha kuuza bidhaa zao kupitia viwandani. Anasema hatua hiyo itasaidia kupunguza hasara na kuinua maisha ya wafanyabiashara katika eneo hilo.

Amebainisha kuwa kwa sasa, zaidi ya tani 10 za matunda huharibika kila siku kutokana na ukosefu wa soko la uhakika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version