News
Wakaazi wa Nyari Wanapinga Uekezaji wa Madini
Wakaazi katika kijii cha Nyari eneo la Sokoke gatuzi dogo la Ganze kaunti ya Kilifi, wanakosoa mpango wa mwekezaji mmoja anayetaka kuchimba madini sehemu hiyo, wakidai kwamba hajahusisha umma.
Wakiongozwa na Thoya Sirya, wakaazi hao wameandamana wakisema wanatilia shaka mienendo ya mwekezaji huyo wa kampuni ya Jalin East Africa Mining ambayo huenda ikawakandamiza.
Wakaazi hao wamemkosoa mwekezaji huyo wakisema amekuwa akishinikiza wakaazi wa sehemu hiyo kutia saini makubaliano bila ya kuwapa mwelekeo wa fidia ya sehemu za ardhi zao.
Kulingana na wakaazi hao, mwekezaji huyo anapanga kuchimba madini aina ya Titanium ambayo jamii inafaa kufaidi kutokana na uekezaji huo.