News

Maelfu ya Watu Wapeana Heshima ya Mwisho kwa Papa Francis

Published

on

Maelfu ya Waumini wa Kanisa katoliki kote ulimwenguni wamepata fursa ya kupeyana heshima yao ya mwisho kwa mwendazake Papa Francis katika Kanisa Katoliki la St. Peters Basilica mjini Vatican.

Mwili wa Papa Francis utasalia katika Kanisa hilo kwa siku tatu kwa ajili ya waumini kuutazama huku maombi maalum yakiendelea kabla ya halfa ya mazishi siku ya Jumamosi Aprili 26 baada ya Misa ya Ibada ya wafu mjini Vatican.

Kabla ya waumini kuruhusiwa kuutazama mwili wa Papa, Kadinali Kevin Farrell ameongoza ibada maalum mapema leo asubuhi baada ya mwili wa Papa kutolewa katika makaazi yake ya Casa Santa Marta hadi Kanisa la St Peters Basilica ukiwa katika jeneza lililo wazi

Maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki wamewasili mjini Vatican kutoa heshima yao ya mwisho kwa mwendazake Papa Francis aliyefariki dunia mnamo siku ya Jumatatu Aprili 21 baada ya kuugua kiharusi.

Viongozi wa mataifa mbalimbali ulimwenguni wakiongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump wanatarajiwa kuhudhuria ibada hiyo ya wafu siku ya Jumamosi, kabla ya mazishi katika Kanisa la Mary Major, nje ya Kanisa la St Peters Basilica.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version