News

Murkomen, Awaonya Maafisa wa Mahakama Dhidi ya Ufisadi

Published

on

Kutokana na kushuhudiwa kwa mizozo ya ardhi ya mara kwa mara katika eneo la Pwani, sasa Wizara ya Usalama wa ndani imewaonya maafisa wa idara ya Mahakama katika kaunti ya Kilifi kukoma kuchochea mizozo ya ardhi.

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, amesema tabia hiyo inafaa kukomeshwa na maafisa wa idara ya Mahakama kuzingatia haki ya kila mmoja wakati wanapotoa agizo lolote kuhusu suala tata la ardhi kwa wakaazi wa kaunti ya Kilifi.

Akizungumza mjini Kilifi wakati wa kikao cha jukwaa la usalama, Waziri Murkomen amesema atafanya mazungumzo na Jaji mkuu nchini Martha Koome kuhusu suala hilo tata ili kuhakikisha maafisa wa idara ya Mahakama ambao wanajihusisha na ufisadi na unyakuzi wa ardhi wanakabiliwa kisheria.

Murkomen amesema sheria imeeleza wazi kwamba mtu yeyote akiishi katika ardhi kwa zaidi ya miaka 12 bila ya usumbufu wowote basi ana haki ya kisheria kupewa hati miliki ya ardhi hiyo, akisisitiza kwamba mizozo ya ardhi Pwani itapata suluhu hivi karibuni.

Wakati huo huo amedokeza kwamba tayari Wizara ya usalama wa ndani, ile ya ardhi nchini, viongozi wa kisiasa pamoja na wadau mbalimbali wanaendelea na mikakati bora ya kuhakikisha suala tata la ardhi kanda ya Pwani linapata suluhu la kudumu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version