Sports
Makala ya mbio za magari WRC kufikia Tamati Jumapili Hii
Maelfu ya mashabiki kutoka afrika mashariki na kati wamiminika mjini Naivasha kaunti ya Nakuru kwa mbio za magari ya WRC Makala ya mwaka 2025.
Kwa mujibu wa waandalizi Zaidi ya mashabiki 30,000 wametua jijini humo kutoka mataifa ya Uganda,Tanzania na Rwanda kwa mbio hizo ambazo zilianza rasmi siku ya alhamisi jijini Nairobi.
Eflyn Evans dereva kutoka taifa la Wales ndio anaongeza akitumia gari aina ya Toyota Gazoo muda sekunde 46.1 baada ya raundi ya pili akifuatwa na bingwa mara mbili Kalle Rovanpera raia wa uhispania akitumia Toyota pia watatu ni Ottok Tanak raia wa Estonia ambaye anatumia gari aina ya Hyundai Shell Mobis.
Dereva anayeongoza mpaka sasa dereva Eflyn Evans na msaidizi wake Scott Martin alikua na haya yakusema baada ya kuchukua uongozi wa mapmea.
“Plan yetu ilifanya kazi vizuri,tunafuraha kuchukua uongozi wa mapema ila bado kazi ipo kwani mizungumzo ni minane,tutaona itakavyokua mpaka siku ya mwisho.”
Kwa upande wake dereva nambari mbili na bingwa mtetezi Kalle Rovanpera na msaidizi wake Jonne Halttunen alisema haya baada ya kushindwa;
“Leo haikua siku nzuri kwetu tulitumia muda mwingi asubuhi ila bado safari ya sisi kurejea kileleni.”
Naye dereva namba tatu Ott Tanak aliyasema haya;
“Hauwezi ukapanga kusema kweli ukiwa hapa kenya vitu vingi vinafanyika,Ni lazima tuketi chini tufahamu tatizo ambalo linatukumba na gari letu.”
Raundi ya tatu na nne yanaishwa maeneo ya Elmentaita huku jumapili mbio hizo zikiisha Hells Gate 1 na Hells GATE 2.
Kilele cha mbio hizo ni siku ya jumapili ambapo rais William Samoei Ruto anatarajiwa kufunga mbio hizo.