National News
Migos Aagiza KNEC, KCPE na KCSE Kuachiliwa Kwa Stakabadhi za Masomo
Wizara wa Elimu nchini Julius Migos amewaagiza wasimamizi wakuu wa shule za upili, msingi na baraza la mitihani nchini KNEC kuhakikisha wanaachilia stakabidhi za masomo za wanafunzi ambazo zinazuiliwa.
Migos amesema hatua hiyo ni sawa na kuhujumu haki za kimsingi za wanafunzi waliofanya mitihani ya kitaifa ya KCSE na KCPE, akisema Wizara ya elimu nchini inafuatilia swala hilo.
Waziri Migos hata hivyo amewataka wakurugenzi wa elimu katika kaunti kuhakikisha wanaandaa ripoti ya agizo hilo katika kipindi cha siku 14, akisema ni lazima wanafunzi hao wapewe stakabadhi zao za masomo.
Kauli yake imejiri baada ya wazazi wa wanafunzi ambao walimaliza mtihani wa kidato cha nne KCSE na wale wa darasa la nane KCPE kulalamika kuzuiliwa kwa stakabadhi za masomo za watoto wao kufuatia visa vya udanganyifu licha ya Wizara ya Elimu nchini kubaini kwamba hakuwa na makosa.