National News
Maafisa wa Afya ya Nyanjani Wapokea Malipo yao, Tanariver
Wizara ya Afya kaunti ya Tanariver, Joshua Jarha, imesema serikai ya kaunti hiyo imewalipa wahudumu wa afya ya nyanjani malimbikizi ya marupurupu yao ambayo wamekuwa wakidai.
Jarha amesema malipo hayo ni marupurupu ya miezi 6, kuanzia mwezi Julai hadi Disemba wa jana na kwamba serikali ya kaunti hiyo inafanya kila juhudi kuimarisha sekta ya afya.
Katika kikao na Wanahabari, Jarha, amesema mikakati mwafaka imeidhinishwa ili kuhakikisha wahudumu hao wa afya ya nyanjani katika kaunti hiyo wanalipwa pesa zilizosalia kwa wakati.
Hata hivyo wahudumu hao wa afya ya nyanjani, wameirai serikali ya kaunti hiyo kuongeza mgao huo wa fedha kwani wamekuwa wakifanya kazi nyingi ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya.