News
Lazima Tufunge Tunisia Magoli ya Mapema, Kauli ya Kocha Odemba Kuelekea Mechi ya Starlets
Mkufunzi wa Timu ya taifa Harambee starlets Beldine Odemba ana amini kwamba uwepo wa mashabiki katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex Ijumaa hii itawapa msukumo timu hiyo wanapojianda kwa mechi ya kufuzu dimba la Afrika AWCON mwakani.
Akizungumza na wanahabari Odemba amesema anasubiri mchezaji wa mwisho kambini Jumatano hii.
“Tuko na karibu full house baada kuwasili kwa wachezaji zaidi ya kumi wa kulipwa,Tunasubiri mchezaji wa mwisho Jumatano hii.” Kocha anazidi kuelezea kwamba, “Lengo letu ni kushinda Tunisia hapa Nyumbani kabla ya mechi ya mkondo wa pili mjini Tunisia Feb 26. Kwa mujibu wa mwalimu huyo na kikosi mchanganyiko Yani chipukizi na wazoefu inampa msukumo kwamba tutaandikisha matokeo chanya, “Wachezaji chipukizi ndio Harambee starlets ya badaye kuwepo kwao kambini inanisaidia kuwa na upana wa kikosi na kujenga kikosi Cha usoni vile vile.Kwa upende wake kiungo wa Besikitas ya Uturuki Cynthia Shilwatso ni kwamba hawataki kujuta Tena baada ya kubanduliwa na Botswana mwaka Jana,” Lengo Letu ni kushinda nyumbani ndio tuenjoy mchezo ugenini, Ni lazima tufunge Tunisia magoli ya mapema kilichotupata mwaka Jana kisitupate tena.”
Kambi ya Harambee starlets imekamilika baada ya wachezaji wa kigeni wote kuwasili kwa pambano la kufuzu dimba la AWCON dhidi ya Tunisia Ijumaa hii ugani Ulinzi Sports Complex mjini Nairobi.
Mechi hiyo itapigwa majira ya saa tisa kiingilio ni shs. 100 mashabiki wa kawaida na shs. 500 watu mashuhuri (VIP).