National News
KEMSA Yazitaka Kaunti Kulipa Malimbikizi ya Madeni ya Jumla ya Shilingi Bilioni 3.5
Mamlaka ya kusambaza dawa nchini KEMSA imezitaka serikali za kaunti kulipa malimbikizi ya madeni ya jumla ya shilingi bilioni 3.5 zinazodaiwa na Mamlaka hiyo.
Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo ya KEMSA, Dkt. Waqo Ejersa, madeni hayo ambayo yamekaa kwa mda sasa yanaathiri utendakazi wa mamlaka hiyo.
Akizungumza na Wanahabari jijini Mombasa baada ya kikao kilichowaleta pamoja wakuu wa KEMSA, Dkt. Ejersa amesema iwapo madeni hayo yatalipwa kwa wakati basi itasaidia Mamalaka hiyo kusambaza dawa kwa wakati hospitalini.
Kauli yake ikiungwa mkono na Mwenyekiti wa bodi ya KEMSA nchini Samuel Tunai, ambaye amesema Mamlaka hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha hospitali za umma nchini zinakuwa na dawa na vifaa vya kutosha huku akisema mpango wa SHA unaendelezwa vyema.