News

Wasichana Pwani wahamasishwa dhidi ya dhulma za kijinsia

Published

on

Wasichana katika ukanda wa Pwani wataendelea kupokea elimu ya kujilinda dhidi ya masuala ya kingono kufuatia mpango wa uhamasishaji, ushauri nasaha na hata michezo.

Mpango huo unawawezesha wasichana kuelewa haki zao na namna ya kuripoti ukatili na jinsi ya kutambua hatari ikiwemo unyanyasaji wa mitandaoni.

Mashirika ya kutetea haki za watoto wa kike yalisema ushirikiano wao na taasis mbalimbali ulirahisisha mpango huo.

Aidha maafisa tawala pia walichangia pakubwa kufanikisha kwa mchakato huo kwani wamewezesha wadau hao kuwafikia wasichana hasa wa mashinani katika ukanda wa pwani.

Wasichana walionufaika kufuatia hamasa hizo wamesema kuwa wamekuwa wakijitwika jukumu la kuwaelimisha wenzao mashinani hasa kuhusiana na swala la hedhi salama na namna ya kuepuka dhulma za kingono mashinani.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version