Entertainment

Wasanii wa Kuimba Wanatabia Nyingi za Kihuni Kuliko wa Hip Hop asema Roma Mkatoliki

Published

on

Msanii wa hip hop kutoka Tanzania anayeishi Marekani, Roma Mkatoliki, amevunja kimya kuhusu kile alichokitaja kuwa dhana potofu inayoambatanishwa na muziki wa hip hop.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Roma alisisitiza kuwa kwa miaka mingi, jamii imekuwa ikiwaona marapa kama wahuni na waasi wa maadili bila sababu ya msingi. Kauli yake imezua mjadala mzito kuhusu mitazamo ya kijamii, hususan tofauti ya namna jamii inavyowaona wasanii wa hip hop na waimbaji wa nyimbo laini.

Roma alisema marapa ni wastaarabu.

“Na sijui ni nani aliwakaririsha hiki kitu. Ukweli ni kwamba tabia nyingi za kihuni wanazo wasanii wa kuimba. Wasanii wa hiphop wengi ni wastaarabu mno,” alisema.

Roma ameeleza kuwa wasanii wengi wa kuimba wanavuta bangi, kunywa pombe, kubadilisha wapenzi kila mara, na kuimba nyimbo zilizojaa matusi na mafumbo ya ngono.

Kwa mujibu wa Roma Mkatoliki ni kuwa wasanii wengi wa hip hop wanaishi maisha yenye misingi ya familia, heshima, na maadili. Wengi wao hawatumii pombe wala bangi.

Roma alitoa mfano wa Nay wa Mitego, Nikki wa Pili, Kala Jeremiah, na Gnako. Zaidi ya hayo, Roma alisema wasanii wa hip hop ndio wanaoongoza kushika nafasi za uongozi ndani ya tasnia ya muziki na hata katika harakati za kijamii.

“Wasanii wengi wa kuimba wanakunywa pombe, tofauti na wasanii wa hiphop. Mtu kama Nay, Nikki wa Pili, Kala I guess na G-Nako hawali tungi kabisa. Wasanii wa kuimba, wengi nyimbo zao zimejaa matusi, ” Roma alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version