News

Wanaharakati wanaitaka serikali kufanya mazungumza na Gen Z

Published

on

Baadhi ya Wanaharakati kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Amina Ridhwan wametoa wito kwa serikali kuu kufanya mazungumzo na vijana wa kizazi cha Gen Z ili kusitisha maandamano ya mara kwa mara nchini.

Wanaharakati hao wakizungumza katika kaunti ya Mombasa, walisema kumekuwa na hali ya wasiwasi nchini hali ambayo inawafanya wafanyabiashara wengi kukosa kufungua biashara zao wakihofia uporaji wa mali zao.

Kulingana na wanaharakati hao ni kupitia mazungumzo kati ya serikali kuu na vijana hao ndipo kutakuwa na utulivu nchini.

“Kwa sababu tunapata watoto wetu wanakufa hakuna maridhiano, hakuna mashauriano kwa hivyo serikali inapaswa kuandaa mazungumzo na vijana hao ili kupatikane mwafaka’’, alisema Ridhwan

Wanaharakati hao pia wamesema baadhi ya vijana wamekuwa wakutumiwa na wanasiasa visivyo ili kuandaa maandamano na kutoa wito kwa vijana kujiepusha na wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi.

“Tutakaa na vijana kwasababu tuko Kenya nzima, sisi hapa tunataka amani ili Kenya iendelee’’, alisema Ridhwan.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version