Business
Wakulima Rabai Wakabiliwa na Hasara Kufuatia Wadudu Kuvamia Mazao
Wakulima wa viazi tamu eneo la rabai kaunti ya kilifi wanakadiria hasara baada ya mimea yao hurabiwa na wadudu.
Kulingana na wakulima hao dawa za kuuwa wadudu ni ghali mno hali ambayo imepelekea wao kushindwa kununua hali ambayo imewsababishia hasara kubwa.
Wakiongea na coco fm hata hivyo wakulima hao wamependekeza wataalam wa ukulima wazuru mashinani kuwaelimisha wakulima jinsi ya kutumia njia za kisasa ili kupata mavuno bora sawa na kuwapa dawa za kukinga wadudu wakisema asilimia kubwa ya wakulima hawana uwezo wa kugharamia dawa.
Aidha wamesema kwamba japo Msimu huu hawatapata mavuno bora,ila wanaimani kuwa asilimia kubwa ya wakulima watavuna ikilinganishwa na misimu ya nyuma kutokana na wingi wa mvua ilivyonyesha msimu huu.