News

Wakaazi walalamikia ukosefu wa umeme Malindi

Published

on

Wakaazi wa eneo la Kajajini mjini Malindi kaunti ya Kilifi wamelaumu kampuni ya usambazaji umeme nchini KPL kwa kutozingatia malalamishi yao.

Wakaazi hao walisema kwa mda wa miezi mine sasa wamekua wakihangaika kupata huduma hiyo ya umeme.

Wakiongozwa na Julius Mweni wakaazi hao walisema kwamba juhudi zao za kumfikia mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo zimegonga mwamba.

Walisema mara kwa mara wamekuwa wakipewa ahadi zisizotimia.

Wakaazi hao waliongeza kuwa hali hiyo imesababisha ukosefu wa usalama huku wakiitaka serikali kuingilia kati.

Vile vile walisema biashara zao zimekuwa zikitatizika kutoka na changamoto hiyo ya ukosefu wa huduma za umeme

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version